Tafuta DHWTangazaTuandikie
Nimejiandaa mwake kiooni!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayewakimbiza na kuwadatisha wabongo ile kinoma...Nakaaya Sumari, amekwishaanza maandalizi kwa ajili ya kushoot video ya pini lake jipya la 'Matatizo'.



Akizungumza na DHW,mwanadada huyo msweetieee kutoka A-Town (Arusha) alidai ameamua kufanya video hiyo ili mashabiki wake wapate kuona picha halisi ya mambo yanayoelezwa ndani ya wimbo huo.

Msanii huyo ambaye kibao chake cha 'Mr Politician' kimemfanya akubalike vyema miongoni mwa jamii...amesema amejiandaa mwake kwa ajili ya shooting hiyo...na kwamba wakati wowote mashabiki na wapenzi watapata kuona vitu vilivyosimama.

Alisema baada ya kuachia albam hiyo na kukubalika kwa kasi..anatarajia kuingia tena chimbo kujifua ili kuwapatia mashabiki wake raha wanayostahili.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.