Ni 3-0 kwenda mbeleeee!
Kundi la Wanaume Halisi, limeendeleza mziki uleule wa 3-0...baada ya kuendelea kulifunika tena kundi pinzanni la Wanaume Family katika maonyesho mawili yaliyofanyika katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu,katika onyesho la Dodoma lililofanyika Ijumaa iliyopita, Wanaume Familiy ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani wakianza na wimbo wa ‘Pisha Njia’, lakini hawakupata support ya kutosha kutoka kwa mashabiki.
Wanaume Halisi walifwatia na wimbo wa ‘Shemeji Shemeji’ ambao uliwachanganya vilivyo mashabiki waliofika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.
Katika hali isiyotegemewa, kundi la Wanaume Family liliwavamia wenzao wa Wanaume Halisi katika klabu ambayo walipata mwaliko wa kufanya shoo usiku huo na kuanza kuwafanyia fujo, ikiwemo kuwatukana matusi ya nguoni na kuwatishia maisha.
Katika onyesho la Morogoro lililofanyika kwenye Ukumbi wa Vijana, mashabiki pia walionekana kuzinguliwa na kundi la Wanaume Halisi kuliko lile la Wanaume Family ingawa walikuwa na wimbo waliotaja mkoa huo ujulikanao kama ‘Dar mpaka Moro’.
Hali ilikuwa mbaya zaidi hata pale walipopanda jukwaani kwa mara ya pili kuimba nyimbo nyingine ambapo mashabiki walikuwa wakiwaonyeshea 3-0 hali iliyodhirisha kwao jinsi Wanaume Halisi walivyo juu.
Aidha, kiongozi wa Wanaume Halisi, Juma Kassim ‘Sir Nature’ amewataka wenzao hao kuacha ugomvi kwani hakuna maana yoyote ila wajipange upya ikiwezekana kutoa nyimbo zilizosimama ili waweze kuwateka mashabiki kama wao walivyofanikiwa.
“Unajua si kama sisi ugomvi hatuuwezi. Tunauweza sana ila sisi tumekuja kufanya kazi, hatujafuata ugomvi ila kama wao wamekuja na mawili sawa, sisi tunafanya muziki na wao wajitahidi kufanya muziki si ugomvi,” alisema Nature.
Hadi sasa tathimini ya ‘Mkali Nani’, inaonyesha Wanaume Halisi kuwa juu zaidi.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala