Tafuta DHWTangazaTuandikie
Nitatumbuiza na Mangaza wa BSS

Yule Kiongozi na muimbaji wa kundi la muziki wa taarabu la Jahazi Morden Taarab Mzee Yusuf, yupo mbioni kufyatua mpini na mshiriki wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS), Mangaza Nyange.



Kiongozi huyo alisema kutokana na kipaji alichokionyesha Mangaza katika BSS, amevutika kufanya naye kazi katika muziki huo wa taarabu.

Yusuf alisema kazi itakuwa nzuri kwani (Mangaza) ameonyesha kipaji cha hali ya juu katika suala zima la uimbaji wa taarabu, sasa ni wakati muafaka kwake kushirikiana naye.

Alisema mpaka sasa ameshaandaa mashairi kadhaa ambayo ataimba pamoja na Mangaza, ili kuwapa wapenzi wa muziki huo ladha mpya kutoka kwa chipukizi huyo.

Mzee Yusuf alisema kufanya kazi na Mangaza ni moja kati ya vitu alivyovitarajia katika dunia ya tarabu hasa kutokana na kuwa na hazma ya kuwasaidia walioonyesha nia ya kutaka kuimba muziki huo.

Mangaza alikuwa ni mmoja katia ya washiriki wa BSS 2008, ambapo mshindi wake alikuwa ni Misoji Nkwabi kutoka Bagamoyo.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.