Wanenguaji DRC hawana lolote-Lilian
Yule mnenguaji nyota wa kundi la Twanga Pepeta International Lilian Joseph Tungaraza 'Internet, asema wanenguaji kutoka mamtoni hususani DRC hawana lolote jipya zaidi ya kuziba riziki.
Mnenguaji huyo alisema kwa mtazamo wake anavyowaona wanenguaji hao, haoni kama wana kitu cha ziada 'jipya' kinachoweza kuwafanya Watanzania wawe na msisimko wa uoga ili waweze kushindwa.
Kwake yeye binafsi anasema kwamba haoni jipya kutoka kwa wanenguaji hao wa mamtoni, kwani kukitokea mpambano wowote ule na wao lazima watawadhibiti.
Alisema ni mara mia hata waimbaji kutoka huko kuliko wanenguaji na hiyo ni kwa ajili ya kuzibitiana riziki tu na si kingine.
Baadhi ya bendi za hapa nyumbani zimekuwa na tabia za kuingiza hata wanenguaji wa kike na wakiume kutoka DRC, katika kile kinachotazamika kuzidi katika ushindani wa anga la muziki wa dansi.
Kwani bendi ya Akudo Impact imekuwa ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanenguaji kutoka DRC, ikifukuzana na bendi ya T-Respect ikiwemo na FM Academia.
Kama wamiliki wa bendi wangetoa nafasi ya kutosha kwa wazawa, basi hawa wageni wangeonekana kwamba hawana lolote.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala