Tafuta DHWTangazaTuandikie
Habari ndo hiyo juu ya Choki

Pablo Masai ambaye ni mwanamuziki katika bendi ya FM Academia, amsifu Ally Choki kwa kumlinganisha na nyota wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC Koffi Charles Olomode pamoja na Papa Wemba.



Mwanamuziki huyo kwa sasa ni kiongozi wa bendi ya TOT Respect na pia ni msanii mkubwa hapa nchini kuliko msanii yeyote kwa sasa.

Masai alisema ukubali usikubali lakini tufahamu kwamba Choki ni mwanamuziki mkubwa, na pia anaweza kumfananisha na mwanamuziki Koffi ama Papa Wemba kutoka Kongo.

Alisema anasema hivyo kwa sababu anajua anachokisema na hata watu wakibisha lakini habari ndo hiyo.

Alisema moja ya kitu kinachowaangusha wanamuziki wa hapa nyumbani ni kushindwa kukubaliana na pale mwenzao anapokuwa na uwezo wa kuweza kukubalika kutoka kwa mashabiki mbalimbali.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.