Jide,TID juuu P/Fame!
Misongi ya wasanii wa Bongo,Lady Jaydee na TID zimetingisha vilivyo jumba la shindano la kutafuta vipaji vya kuimba linaloshirikisha nchi za Afrika Mashariki linalofanyika Nairobi, Kenya.
Songi za wasanii hao zimeweza kuchaguliwa kwa zaidi ya mara moja katika shindano hilo.
Songi hizo ambazo ni 'Siku Hazigandi' na 'Mawazo za Jaydee' na 'Siamini' na 'Zeze' za TID ziliweza kufanywa vyema baada ya kuweza kuimbwa kiufasaha na washiriki kutoka Kenya na Uganda.
Katika mchakato huo washiriki walitakiwa kuimba nyimbo za nchi nyingine, mfano mshiriki kutoka Tanzania alitakiwa kuimba nyimbo kutoka Uganda au Kenya.
Washiriki wanne kutoka Kenya na Tanzania waliimba nyimbo za wanamuziki Jaydee ambazo ni Mawazo, Siku Hazigandi, Zeze na Siamini na kuwafanya kuwa wasanii pekee kutoka Tanzania ambao nyimbo zao zimesikikia zaidi ya mara moja.
Shindano hilo lilianza Aprili 13 likiwa na washiriki 15, watano kutoka Tanzania, watano kutoka Uganda na watano kutoka Kenya.
Tayari washiriki watatu kutoka Kenya Uganda na Tanzania wamekwishayaaga mashindano. Nao ni Arthur Kiwala ( Uganda, Valentino Mwakasoke (Tanzania) na Irene Karanja (Kenya).

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala