'The Dudu' mkatabani!
Baada ya mengi kusemwa juu yake,hususan kuhusu kufa kwake kimuziki...msanii Godfrey Tumaini 'Dudubaya' amesignmkataba na Kampuni la Art in Tanzania...litakalokuwa na jukumu la kusimamia kazi zake za kimuziki.
Hayo aliyathibitisha mbele ya meza yetu,ambapo alidau kuwa moja ya majukumu ya kampuni hiyo itakuwa ni kusambaza albamu yake na kumtafutia matamasha mbalimbali nje ya nchi.
Kwa mujibu wa mujibu wa Dudu,albam yake mpya aliyoipa jina la 'Mamba' imekamilika na itakuwa mitaani wakati wowote na kuwataka mashabiki wake waisubiri.
"Wapenzi wangu wakae mkao wa kula kwani albamu yangu iko jikoni na muda wowote kuanzia sasa itatoka ikiwa na vionjo tofauti na vile vilivyozoeleka na ninaamini wote wataburudika," alijigamba Dudubaya.
Pia, alisema kampuni hiyo imeandaa mavazi yenye nembo inayomtambulisha msanii huyo ya 'Mzuka' ambayo itakuwa kwa njia ya T-shirt, kofia, vipeperushi na zitauzwa katika maduka yaliyoko Coco Beach na katika ofisi za Art in Tanzania.
Alizitaja baadhi ya nyimbo zilizo katika albamu hiyo kuwa ni Jumba, Nitawaua, Welawela remix, Sambusa, Mola, Ukweli, Wewe na Mzuka.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala