Tafuta DHWTangazaTuandikie
Daz Nundaz Chali!

Baada ya kufukuzwa Daz Baba kwenye kundi lake la zamani la Daz Nundaz..kwa maelezo kuwa anatabia zisizoridhisha ikiwemo utukutu na kujihusisha na madawa ya kulevya,msanii mwingine kutoka kundi hilo maarufu kwa jina LaRhumba naye amejiengua rasmi na kujiunga na Daz Baba.



Hayo yalithibitishwa na wasanii hao wawili mwishoni mwa wiki...ambapo walisema tayari wameunga nguvu na kuanzisha kundi jipya liitwalo 'Tanzaniano' ambalo litajumuisha wasanii watatu akiwemo yeye...Daz Baba,LaRhumba pamoja na kichwa kingine hatari kilichotajwa kwa jina la Ali Mbongo.

Akielezea kilichomwondoa ndani ya kundi lake hilo la zamani.....LaRhumba alisema kimetokana na maslahi duni...na kumtupia lawama kiongozi wa kundi hilo...Ferooz...kuwa amekuwa akijimegea mkwanja mwingi kwenye kazi za kundi hilo na kuwapunja wenzake..jambo ambalo alisema halijakaa sawia.

Mpaka tunakwenda mitamboni...'Tanzaniano' waliidodosea DHW kuwa tayari wamesharelease songi lao jipya linaloitwa 'Model Tanzania'.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.