Mkongwe Bozi Boziana kuja Tz
Yule mkongwe wa muziki wa bolingo barani Afrika kutoka nchini Congo Bozi Boziana, anatarajia kuja nchini kukonga nyoyo za watanzania kwa kupamba uzinduzi wa albamu ya Akudo Impact.
Uzinduzi huo utalipuka Mei 16 hapa hapa nyumbani ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkongwe huyo atawasili hapa nchini Mei 13 akifwatana na wanamuziki 17, kwa ajili ya uzinduzi wa albamu hiyo iliyopewa jina la Impact.
Mbali ya mzee Bozi Boziana uzinduzi huo pia utapambwa na kundi linaloongoza hapa nchini kwa miondoko ya taarab 'kidole juu', Jahazi Modern chini ya Mzee Yusuph.
Bendi ya Akudo itafanya onyesho lake la mwisho Mei 4 ndani ya ukumbi wa Msasani Beach Club, na baadaye kuingia kambi ya wiki mbili kujiandaa na uzinduzi huo.
Albamu ya Impact imebeba jumla ya nyimbo nane ikiwemo ya 'Safari Siyo Kifo', 'Crazy Love', 'Inauma Sana', 'Maisha' na wimbo ambao unatamba sana hivi sasa ujulikanao kwa jina la 'Yapo Wapi Mapenzi'.
Nyimbo nyingine ni pamoja na Huruma, Binadamu na ule unaobeba jina la albamu hiyo, Impact.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala