Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni B-CONNECTED May 17!

Tamasha la muziki la kimataifa la B-CONNECTED ambalo hurindima kila mwaka,linatarajiwa kufanyika tarehe 17 May kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dsm kama iliyo ada yake.



Mtamasha huo kwa kawaida huwakutanisha wasanii wachanga na waliobobea kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Bongo,Uholanzi na Afrika Kusini wanaofanya miondoko ya muziki wa kizazi kipya pamoja na reggae.

Taarifa iliyoifikia meza ya DHW..ilisema kuwa mchunjo kwa wasanii chipukizi wa Bongo watakaopanda jukwaani kufanya makamuzi siku ya Tamasha hilo bado unaendelea na washindi watapatiwa mafunzo mahsusi ya namna ya kuandika nyimbo zenye ujumbe mzuri wa ukimwi.

Tamasha la aina hii ambalo linajulikana zaidi kiutaalam kwa jina la 'Open Mic' limeandaliwa na shirika la Music Mayday Tanzania na kudhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali la Family Heath International (FHI),Ubalozi wa Uholanzi, True vision production na Hivos.

Tamasha hili linafanyika kwa mara ya tano kwa hapa Bongo likiwa katika harakati ya kuwasaidia vijana wenye vipaji katika muziki na sanaa .

Ukiachilia mbali wasanii chipukizi wanaotafutwa kuperform siku hiyo,mastaa watakaopanda kwa upande wa Bongi ni pamoja na FID Q, Nako2nako, Nakaaya na wengine wengi. Kutoka Uholanzi watakuwepo kundi maarufu la Reggae la Roots riders au Tribute 2 Bob Marley.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.