Na2mia 'Akili Yangu' masela!
Msanii MB Dog,ambaye wengi mtaani wanamtambua kama
gwiji la miondoko ya sauti za kutokea puani,...ambalo miezi michache tu iliyopita liliamua kujitoa kwenye familia ya 'Tip Top Connections' iliyomlea na kumfikisha kwenye chart za juu na kuamua kufanya kazi kivyake...yu tayari kuachia albam yake mpya.
Hayo aliyathibitisha na yeye mwenyewe...mwanzoni mwa wiki...ambapo alidai ukimya wake wa takriban miaka miwili tangu atoke na albam yake ya kwanza...huenda ukaisha very soon....kwani albam yake mpya inakuja ikiwa na jina la 'Akili Yangu'.
Akifafanua ni kwanini aliamua kuipa albam yake jina hilo...Mb Dog..alisema wazo hilo limetokana na yeye kujiona amekwishaiva vya kutosha kimuziki na ndio maana akaamua kutoka kundini na kuamua kutumia akili yake kujitegemea.
Mb Dog,aliendelea kwa kusema kuwa mpaka sasa amesharekodi jumla ya track 24...na kwasasa ana mtihani mkubwa wa kuchagua track 12 zitakazoingia kwenye albam hiyo mpya.
Hadi tunakwenda mitamboni alikuwa anajiandaa kurelease pini lake jipya liitwalo 'Natamani' ambalo kazi ya utengenezaji wake imefanyika kwenye studio za 41 Records chini ya Producer Ambrose a.k.a Dunga.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala