Tafuta DHWTangazaTuandikie
Tz wanabendi zilizokwenda shule

Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta Original', yawakonga Wakenya nyoyo zao kwa burudani nzito waliyoionyesha.



Naye Rais Mwai Kibaki wa Kenya alisema bendi hiyo iliweza kuwapagawisha wananchi wa nchi yake, kwa kulisakata rumba la aina yake.

Bendi hiyo kwa sasa iko Kenya kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo, na iliweza kutumbuiza ndani ya Viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi.

Mbali na Rais wa nchi hiyo pia Makamu wake Kalonzo Musyoka, pia naye aliweza kupagawishwa na mipini iliyokuwa ikikung'utwa kwenye bendi hiyo.

Nyimbo zilizoonekana zaidi kuwateka Wakenya akiwemo Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi, ni pamoja na 'Africa Unite' pamoja na 'Mtu Pesa'.

Nyota wa bendi hiyo walio onyesha uwezo wao wa hali ya juu ni pamoja na Charles Gabriel 'Chalz Baba', Saleh Kupaza, Hamisi Amigolas, Luiza Mbutu 'Mama B'akiwemo na Khalid Abeid Chuma 'Chokoraa' aliyetesa kwa rapu zake katika onyesho hilo.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.