Tafuta DHWTangazaTuandikie
Hatimaye Nyoshi kuparamia jukwaa la Twanga

Kiongozi wa bendi ya muzikiwa dansi ya FM Academia Nyoshi el Saadat, wiki iliyopita aliweza kuibuka kwa ghafla ndani ya ukumbi wa Deep West.



Mwimbaji huyo aliweza kuvamia jukwaa na kuanza musalimiana na waimbaji wa bendi hiyo, mmoja baada ya mwingine na hakikufahamika kitu kilichompeleka Kenya ni nini.

Ndani ya ukumbi huo wa Deep kulikuwa na bendi pinzani ya African Stars 'Twanga Pepeta' iliyokuwa ikitowa burudani siku hiyo.

Bendi ya Twanga ilikuwa hapa nyumbani kwa kuadhimisha sherehe za siku ya wafanyakazi duniani, baada ya kualikwa na Chama cha Wafanyakazi cha hapa nchini.

Iliweza kufanya onyesho lake nyakati za mchana ndani ya viwanja vya Uhuru Park, kwani mamia ya watu walikuwa nyomi.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.