Tafuta DHWTangazaTuandikie
Utata waibuka Project Fame!

Noma kubwa ilitokea hapo juzi ndani ya jumba la Tusker Project Fame kati ya majaji, walimu, mashabiki na watangazaji. Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya shindano hilo, mvutano huo umetokea baada ya majaji kutangaza majina ya washiriki wanne ambao wako katika hatua ya kupigiwa kura ya mshiriki mmoja kutolewa katika shindano hilo.



Walimu na mashabiki walikuwa wakipinga hatua ya kuwachagua washiriki hao kwa madai kuwa wamewaonea kwani kuna wengine wameonyesha kiwango kizuri na kuwa haiwezekani wanawake peke yao ndio waonekane wakiimba vibaya.

Hata hivyo, mtangazaji wa shindano hilo, Gaitano Kagwa aliwasihi majaji kuwa makini wakati wanapowapendekeza washiriki wa kuwatoa kwani wanaweza kutoa mshiriki aliye bora na kumuacha mshiriki ambaye hastahili chochote.

Kitendo hicho kilimfanya mmoja wa majaji,Ian Mbugua kumtaka Gaitano asiingilie kazi ya ujaji na anyamaze kimya kwani wao kama majaji ndio wenye uamuzi wa mwisho....kitendo ambacho hakikumridhisha Gaitano.

Kimbembe hicho kilifikia wakati....Jaji Mbugua...alipoamua kumwita Gaetano mjinga na awaache wafanya kazi yao...kauli hiyo iliwakera mashabiki wanaohudhuria shindano hilo ambapo waliamua kupiga kelele za kumtaka jaji huyo aondolewe.

Hata hivyo, Watanzania wawili wamependekezwa kupigiwa kura za kutoka kwenye shindano ambao ni Linah Mohammed (9) na Asha Mashauri (2) ambaye alinusurika wiki iliyopita baada ya washiriki wenzake kumtaka abaki. Kutokana na kupendekezwa kwa mara ya pili Asha aliangua kilio akiwa kwenye jukwaa. Washiriki wengine ni Wakenya Alice Waweru (1) na Wendy Kimani (14).


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.