Asha abwaga minyanga!
Baada ya mikanganyiko kadhaa kutokea ndani ya shindano la Tusker Project Fame.......hatimae mshiriki wetu kutoka Bongo..Asha Ramadhani,ameamua kujitoa ndani ya shindano hilo linaloshirikisha nchi za Afrika Mashariki.
Mwanadada huyo aliamua kujitoa hapo majuzi wakati tayari akiwepo kwenye listi ya wasanii wanaotakiwa kutolewa hii ikiwa ni wiki yake ya pili mfululizo.
Kujitoa kwa Asha....kuliungwa pia mkono na madaktari waliowapima afya wasanii hao kabla ya kuingia ndani ya jumba hilo...wakisisitiza kuwa huenda ikawa imechangiwa na msongo wa mawazo uliotokana na ushindani mkali.
Wakati akiondoka Asha alisema: " Nawashukuru wote walionipa ushirikiano wao na kuwashukuru wote walionipa nafasi ya kushiriki Tusker Project Fame.”
Mtanzania huyo aliangua kilio Jumapili baada ya kutajwa katika orodha ya washiriki wanne wanaotakiwa kupigiwa kura, washiriki hao walirudi ndani ya jumba jambo ambalo lilimfanya Asha kuwa na mashaka.
Waangalizi wa jumba hilo walilazimika kumkimbiza Asha Hospitalini na akiwa huko alifikia uamuzi wa kujitoa kwenye shindano, uamuzi ambao uliungwa mkono na madaktari wanaoangalia jumba la Project Fame.
" Tunasikitika na uamuzi wa Asha wa kuondoka kwenye shindano lakini tunamtakia kila la heri si katika muziki tu bali pia katika maisha yake.
“ Tumejikitika katika kuibua vipaji katika nchi tatu za Afrika Mashariki lakini pia tunaheshimu uhuru wa mshiriki kufanya maamuzi yake. Tutaendelea kumsaidia na washiriki wengine kuhakikisha wanatimiza ndoto zao,” alisema bondi ya wakurugenzi ya Tusker project Fame.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala