Pinda kupekecha na Akudo!
Mheshimiwa Waziri Mkubwa...Mizengo Pinda...anajiandaa kwa makamuzi makali kusakata pekecha pekecha siku ya uzinduzi wa albamu ya bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact (Wazee wa Masauti) utakaofanyika Mei 16, mwaka huu.
Akichonga na waandishi hapo jana,Mratibu wa uzinduzi huo, Bahati Singh alisema katika uzinduzi huo ambao Waziri Mkubwa ndiye atakayekuwa Mgeni Rasmi, bendi hiyo itasindikizwa na mwanamuziki kutoka Kongo, Bozi Boziana na Jahazi Morden Taarabu na utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Wazee wa Masauti...ambao wamekuwa tishio kubwa bendi zingine hapa town...tayari wamekwishaahidi burudani ya kukata na shoka, ambapo wapenzi wataulizwa kama ni funika bovu au la, kama burudani haitakonga nyoyo za mashabiki, hiyo ndio itakuwa mwisho wa bendi ya Akudo," alisema Singh.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala