Albam sasa June - Chokoraa
Ule uzinduzi wa albam binafsi ya muimbaji nyota wa kundi la African Stars "Twanga Pepeta International"... Khalid Chuma maarufu kama Chokoraa.... sasa umepangwa kufanyika June 5 katika ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es laam.
Awali uzinduzi wa albamu iitwayo 'Kuachwa', ulikuwa ufanyike mwezi uliopita lakini ulishindikana kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa takriban siku nzima ya onyesho hilo.
Kwa mujibu wa Chokoraa sasa uzinduzi huo utafanyika kama ilivyopangwa upya bila wacwac wowote na kwamba wasindikizaji watakuwa walewale waliokuwa wamsindikize ktk uzinduzi ulioahirishwa...na kuwataja baadhi kuwa ni TID pamoja na Bendi za Twanga Pepeta,FM Academia bila kuwaahau wazee wa masauti Akudo Sound.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala