Tafuta DHWTangazaTuandikie
FA azushiwa kifo!

Msanii Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA a.k.a Binamu .....ambaye amekuwa gumzo kubwa ktk siku za karibuni kutokana na pini lake 'Bado niponipo kwanza' amezushiwa kifo.



Habari hizo za uzushi zilizoenea jijini kwa spidi ya ajabu na hata kuripotiwa na baadhi ya mitandao,zilisababisha waandishi wetu kutumia nguvu ya ziada kusaka ukweli....na kuamua kumgongea msanii huyo kwenye simu yake ya mkononi na kukuta haipatikani kwa wakati huo.

Jambo hilo liliendelea kumpa wasiwasi mwandishi wetu na kuamua kumgongea mshkaji wake wa karibu ambaye mara baada ya kumuuliza kuhusu taarifa hizo aliangua kicheko cha ajabu na kuziita habari hizo za uzushi kwani alikuwa ametoka kuonana na FA muda mchache tu uliopita.

Baada ya kujiridhisha na taarifa hizo timu ya DHW ilikaa chini na kujuliza bila kupata majibu..je ni nani haswa anayevumishaga uzushi huuu...maana hii sio mara ya kwanza wasanii wa Bongo kuzushiwa kifo huku wakiwa fiti kabisaaaaaa!


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.