Malkia wa Sebene 2008 kunukia
lile Shindano la kumsaka malkia wa Sebene linatarajia kuibuka tena, ndani ya mwaka huu hapa hapa jijini.
Kwani washiriki walioshiriki mwana jana hawataruhusiwa tena kupanda ndani ya jukwaa.
Naye Mratibu wa shindano hilo lililopata Justine Jones alisema kwamba, shindano hili litafanyika Desemba mwaka huu.
Jones alisema nia ya kutoruhusu washiriki wa zamani ni kuwaachia uwanja washiriki wapya, hasa zaidi wasichana wanaochipukia na kipaji cha kucheza.
Alisema mwaka huu wameboresha zaidi shindano lao, kuanzia zawadi na mfumo mzima wa uendeshaji tofauti na mwaka jana.
Tofauti na mwaka jana ambapo mshindi alipewa zawadi ya gari, washindi wote mwaka huu watapewa zawadi za pesa ili kuwasaidia katika maisha ya kijasiriamali.
Kuhusu maandalizi alisema yanaendelea vizuri ambapo fomu zimeshaanza kutolewa kwenye ofisi za bendi ya FM Academia, na mwisho wa kurejesha ni wiki mbili zijazo kuanzia sasa.
''Yeyote mwenye kipaji cha kucheza, umri usiopungua mika 18 ana ruhusiwa kushiriki bila kujali anatoka mkoa gani, aliseama zaidi Jones wa kampuni ya Tan Vision Limeted.
Katika shindano hilo, bendi ya FM Academia inayojulikana zaidi kama 'Wazee wa Ngwasuma watakua jukwaani kutumbuiza .
Mshindi wa mwaka jana alikuwa kimwana Ketura Kiongosi aliyeshinda zawadi ya gari, Toyota Mark ll (Baloon).

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala