Tafuta DHWTangazaTuandikie
Jumbe kuunda bendi yake

Si mwingine bali ni yule nguli wa miondoko ya dansi hapa nchini Husseni Jumbe, kwa sasa yupo mbioni kuunda bendi yake binafsi.



Ila ataendelea kuwepo ndani ya bendi yake ya sasa ya Msondo Ngoma.

Jumbe alisema kwa sasa yupo kwenye harakati za mwisho za ukamilisha taratibu za kuunda bendi hiyo.

Jumbe alidokeza kuwa tayari ameshawanasa baadhi ya wana muziki toka bendi mbalimbali, atakaofanya nao kazi ndani bendi yake hiyo mpya.

Alisema ukimya wake ni kumaliza albamu yangu binafsi, kwani kwa sasa yuko mbioni kuunda bendi yake binafsi ambayo itamsaidia kuniingizia kipato.

Mtunzi na muimbaji huyo mahiri aliyewahi kuzipigia bendi mbalimbali hapa nchini na Kenya, zikiwemo DDS Mlimani Park, TOT _ Plus na Mikumi Sound alikuwa katika maandalizi ya kutoa albamu yake binafsi ya tatu.

Tayari alishafyatua mipini mitatu ya Ulevi,Kijakazi na Harusi aliyoirekodi kwenye Studio ya Sound Crafters, kwa miondoko ya Zouk na Rhumba akiwashirikisha wanamuziki mbalimbali.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.