Tafuta DHWTangazaTuandikie
Jahazi Uingereza Des. 13

Kundi zima la miondok ya kidole juu Jahazi Modern Taarab, linatarajia kukonga nyoyo za Watanzania wengine London katika sherehe ya sikukuu ya Uhuru.



Sherehe hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa Wembely Decemba 13 mwaka huu.

Naye Mkurugenzi wa Masoko ya kampuni ya Jambo Publications iliyoratibu onesho hilo, kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania Uingereza ,Juma Makabkila alisema maandalizi yote ya onesho hilo yamekamilika na iliyobaki ni siku yenyewe kuwadia.

Mbali na Jahazi onesho hilo litapambwa na msanii Vicky Kamata, ambae atatambulisha nyimbo zake zilizopo ndani ya albamu yake mpya inayotarajia kutoka hivi karibuni.

Vicky ni msanii aliyejipatia sifa kubwa Tanzania, lakini hivi sasa hivi anasoma huko London.

Kundi zima la Jahazi lenye wasanii 14 linatarajia kuwasili nchini Decemba 9, tayari kwa onesho hilo.

Kwa sasa kundi hilo linafanya taratibu la onyesho hilo la tarehe 13, na maonesho mengine bado hayapo kwenye programu yao.

Wanamuziki wanaokuja na kundi hilo ni pamoja na kiongozi Nasibu, Leila Abdallah, Fatuma Masoud, Miraji Mohamed, Musa Mkenda Musa, Jumanne Ulaya,Fikirini Urembo, Rashid Nassoro na Isha Makongo.

Kundi la Jahazi hivi sasa linatamba na nyimbo zake kama kazi ya Mungu haiingiliwi, nakula kwa nakshi nakshi’, Sichoki kustahamili, Shukrani ya punda,Katu hatorudi kwako, nimemshika habanduki, mtasema sana lakini hapa ndio amefika na nyingine nyingi.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.