FM na Video mpya
Kwa sasa inajidai na video ya wimbo wa 'Heshima ya Mwanamke' na sasa inaamua kuweka nguvu zake kwa upande wa pili wa Vuta Nikuvute ili uweze kuonekana katika video.
Unaweza kujiuliza maswali mengi na ukakosa majibu kwamba hawa ni kina nani, si wengine bali ni wale wakali wa dansi hapa nchini FM Academia.
Kelvin Mkinga ambaye ndiye msemaji wa bendi hiyo alisema kwamba bendi hiyo inatarajia kuingia mzigoni kuanzia wiki hii, kwa madhumuni ya kuandaa video yao katika maeneo mbalimbali ya hapa nyumbani.
Mbali na hilo mbendi hiyo itaendelea kwa kufanya makamuzi ya kushuti video ya wimbo huo mishale ya mchana, huku usiku ikiendelea kama kawaida kulipua burudani sehemu mbalimbali hapa jijini.
Alisema wimbo huo unatarajia kwenda sambamba na rapu mpya ya Kula Kidogo Acha Kidogo.
Bendi hiyo imekuwa ni moja kati ya bendi za mashabiki topu kwani imefanikiwa kujizolea mashabiki kibao ukilinganisha na bendi nyingine za hapa nchini.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala