Twanga na moto wa kifuu!
cya dansi hapa nchini, inatarajia kuwashika wapenzi wake wa miondoko hiyo ya kudansi dansi ndani ya ukumbi wa Basi Haya Campsite uliopo jijini.
Naye mwimbaji nguli wa bendi hiyo Khalid Chuma 'Chokoraa', alisema bendi hiyo inatarajia kuwapagawisha wakazi wa Boko kwa staili zake mpya za 'Sugua Kisigino' ya Saulo Ferguson na Kidude ya Chokoraa.
Rapa huyo alisema bendi ya Twanga Pepeta itaangusha moja moja katika onyesho linalotarajiwa mishale ya usiku wa kuanza saa 3:00, huku wakiporomosha nyimbo mpya zinazotarajiwa kuwamo kwenye albamu ya 10 ya bendi hiyo hapo mwakani.
Baadhi ya nyimbo hizo zitakazoangushwa ni pamoja na unaotamba sasa wa Sumu ya Mapenzi, Mtoto wa Mjini Nazi Haivunji Jiwe.
Rogart Katapila na pia Msafiri Said 'Diouf' aliyekuwa rumande hivi karibuni, atatambulisha rap mpya za Weka Selo na Mambo Maregea.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala