Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ndanda na Watoto wa Tembo

Gwiji wa muziki wa dansi hapa nchini Ndandason Ngongo ‘Ndanda Kosovo', ameweza kuja kivingine na bendi ijulikanayo kwa jina la Watoto wa Tembo International.



Akilonga na mwanadarhotwire ndani ya ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa hapa jijini, Mkurugenzi wa bendi hiyo Jane Mawole alisema kwamba bendi yake inaundwa na wanamuziki wapatao 18.

Alisema wengine wanaounda bendi hiyo ni pamoja na waimbaji wanne, marapa wawili, wapiga vyombo sita na wacheza shoo watano.

Bendi hiyo inatarajia kuingia kambini siku chache za usoni kwa ajili ya kujifua, na inatarajia kuingia kambini miezi minne katika miji ya Mikumi Morogoro na Arusha.

Alisema kuwa baada ya kimya cha muda mrefu bendi hiyo mpya itafanya makamuzi yake rasmi Desemba 8 mwaka huu, katika ukumbi wa New Muafaka Social Club, ulioko Mbezi Beach nyuma ya Art Galley.

Bendi hiyo itaanika vibao vyake vikiwemo Afrika Yetu, Usitoe Mimba, Uniache, Kosivo Kiboko ‘Jambembe’, pamoja na 'Cecika'.

Siku hiyo mashabiki watajionea staili mpya ambayo imetoka Mikumi, ijulikanayo kwa jina la ‘Lilolo’ na nyingine ya ‘Swala-Ka-Lakaswa.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.