Lord alambwa Pingu akitengeneza mkoko!
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ anayepiga mzigo kwenye Kundi la Nako2nako, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akitiwa pingu na askari wa doria baada ya kumshuku kuwa ana bangi ndani ya gari lake.
Tukio hilo lilitokea pande za Kinondoni kwenye gereji moja karibu na Baa ya M.K, ambako Lord Eyez alikuwa na demu wake Rehema Chalamila ‘Ray C’ wakitengeneza gari yao ghafla mbele yao lilitokea gari la askari hao na msanii huyo akapandisha kioo cha gari haraharaka ili asionekane.
Kitendo hicho kiliwapa wasiwasi askari hao waliokuwa na gari ya doria na kutafasiri kuwa mwanahip hop huyo alikuwa na kitu cha kihalifu ndani ya gari hilo ndipo walipoamua kumfuata kwa lengo la kumkamata na kwenda kumkagua kituoni.
Askari hao walifanya upekuzi kwenye gari lake na hawakubaini kitu, ndipo wakamwamuru Lord Eyez kwenda naye kituo kidogo cha polisi Mwananyamala Mwinyijuma, kumfanyia upekuzi zaidi.
Mchizi aligoma kupelekwa kituoni na ndipo askari hao wakaamua kumtia pingu, kisha kuondoka naye lakini hatahivyo hawakumkuta na bangi na kuamua kumwachia huru.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, kitendo cha Lord Eyez kukamatwa na kupelekwa kituoni kilimkera Ray C ambaye walikuwa pamoja na muda mwingi alionekana akimtupia lawama fundi wa gari hilo ambaye alichelewa kumaliza kuifanyia matengenezo ndinga yao ambayo imekuwa ikiwasumbua mara kwa mara.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala