Extra Bongo meno nje
Imeweza kufanikiwa kupata vyombo vipya viloivyogharimu zaidi ya Sh. Mil 30, na vitazinduliwa rasmi hapo Februari 14 mwaka huu Siku ya Wapendanao 'Valantine Day'.
Si nyingine bali ni ile bendi ya Extra Bongo 'Next Level', na bendi hiyo inaongozwa na Ally Choki na ilikuwa ikitumia fedha nyingi kwa kila onyesho ili kulipia vyombo vya kukodi kwa zaidi ya miezi sita sasa tangu ifufuliwe.
Msemaji wa bendi hiyo, Douglas Sagawala, alisema tayari vyombo hivyo vimeshawasili nchini kutoka Uarabuni kupitia bandari ya Zanzibar.
Alisema hafla ya uzinduzi wa vyombo hivyo itafanyika ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, sambamba na shoo ya kuwaburudisha wapendanao.
Bendi hiyo iko katika harakati za kuitangaza albamu yake ya kwanza inayojulikana kwa jina la ‘Mjini Mipango’, ikiwa na mipini sita.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala