/td> Tafuta DHWTangazaTuandikie

Darhotwire.com haitahusika na maoni ya msomaji yeyote aliyotuma katika ukurasa huu kuhusiana na story zetu.

Abiria na zogo la nauli za mkoa


Majembe keep it up, tumechoka kuonea, SUMATRA hongereni sana kwa kuwaweka MAJEMBE kushughulikia hizi kero. Kweli viongozi mumeona mbali kwenye hili suala la kuanzisha Majembe, kinachotakiwa hawa MAJEMBE Wasiendekeza uzembe, FANYENI KAZI!!!
BLESSES OF MY BELOVED LIVING GOD BE UPON YOU.

* Comment by Juma Jaredi
* Date Thursday, December 24, 2009
View Original Story

Ahsante Darhotwire kwa kutupa habari motomoto kila kukicha. Pamoja na ukweli huo, ningependa kushauri waandishi wa darhotwire wazingatie utumiaji sahihi wa maneno ya kiswahili. Mwandishi wa habari hii anaonekana kukosa kabisa ufahamu wa namna ya kupangilia mtiririko wa habari na hata mpangilio wa maneno.

Kwa mfano, Mwandishi ametumia neno "Kwani" pasipo stahili na pia kuna makosa kadhaa ya maneno kwa mfano neno"huku" limekosewa na kuandikwa "uku". Kuna makosa mengi sana ya kiandishi kwenya habari hii hususan paragraph ya 1,2,3,7,8, na 11.

Sina hakika kama mhariri wa darhotwire anafanya kazi yake ipasavyo kwa sababu makosa ya uandishi yapo katika kila habari ya darhotwire.Huenda pia darhotwire inahitaji kuwaelimisha zaidi waandishi wake kwani wanaonesha uwezo mdogo sana wa taaluma hii.

Kila la heri na ninawatakia heri ya Christmas na Mwaka mpya!

* Comment by Jafary Fafara
* Date Friday, December 25, 2009
View Original Story

Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kila kitu kwani kama sio yeye siku hii kwangu ingekuwa ndoto.Nashukuru pia kwa nafasi hii ya pekee ya kutoa maoni au mtazamo wangu kwa suala hili la nauli.Ni vigumu sana kumsimulia mtu utamu wa asali akakuelewa.Ili umalize utata itabidi tu umtafutie asali naye aionje.Viongozi na watu wenye uwezo wengi hawatumii usafiri tunaoulalamikia,unafikiri wataguswa na shida zetu.Muda umefika sasa wa kila mtu kutambua sheria za nchi ili uweze kutambua haki zako.Sheria za nchi yetu zipo kwa ajili ya wanyonge yaani watu wa chini tu.Wale wasio nacho sheria hufanya kazi tena kwa nguvu zote ukilinganisha na wale walio nacho.Hebu jiulize kama ni wewe gari lako limegonga mtu tena halina leseni ,nakwambia unaozea jela ila mheshimiwa wala.Sheria zetu zimebakia kwenye makaratasi na kama ni kufanya kazi basi ni kwa watu wa chini ndio wanaumia.Nashangaa sana mtu anakiuka mkataba au sheria ya huduma halafu mnasema atatozwa faini,Hii haisaidii kitu .Mfano Nimefanya biashara ya faida ya shilingi milioni mbili unanitoza faini ya laki mbili hii sishindwi kulipa.Ila mtu huyu ukinyang'anywa Leseni na kuwapatia wazalendo wenye uchungu na nchi yao mambo haya yatakoma.wakati huo huo mahakama ikasimamia haki basi kila itu kitakuwa sawa.Hivi mimi nashindwa kuilewa nchi yangu hata sasa nachanganyikiwa,suala la rushwa unahitaji tume?waziri wa sheria ambaye nadhani sijui kama yupo,mheshimiwa si uende mahakamani ujionee mambo?Fanyeni kama marehemu Sokoine nenda bila taarifa utashangaa.Polisi siku hizi unakwenda na daftari lako la kuandikia RB,kuna baadhi ya nyaraka zingine ukifika unaambiwa ukagurudubishe kama unataka huduma,kumbuka hapa nipo na mtu amejeruhiwa na damu zinamvuja kwa wingi lakini unaambiwa ukagurudubishe makaratasi.Sasa kweli kama sio dhuluma kodi inakwenda wapi?Hivi ninapokwenda kuhuisha leseni yangu ya gari kisha unanipa makaratasi fulani nikagurudubishe ndiyo nipate huduma.Je hiyo kodi ninayolipia haijumuishi na makaratasi unayoniambia nikagurudubishe?Hebu teamke sasa.

* Comment by Mollel
* Date Tuesday, December 29, 2009
View Original Story


Archive:

Copyright © 2010 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.