Darhotwire.com haitahusika na maoni ya msomaji yeyote
aliyotuma katika ukurasa huu kuhusiana na story zetu.
Maghembe na mkazo mzito juu ya Elimu ya dunia kwa Waislamu
Ni elimu ipi hiyo anayoisemea Mheshimiwa?Nafikiri ni muda muafaka wa kila mtanzania kufikiria wapi tunaelekea hasa katika wakati huu ambao tabaka la matajiri na masikini limekuwa likiongezeka kila kukicha.Sidhani kama elimu ya Dini haina maana au nafasi katika maisha yetu.Professa anasahau Elimu aliyoipata ilikuwa FREE kama sio bure.Kusomesha mtoto katika kipindi hiki kwa maisha yetu ya kawaida nafikiri wewe mwenyewe ni shahidi.Nafikiri kumfundisha mtoto amtumainie mwenyezi MUNGU ni kitu bora zaidi ya Uprofessa bila Mungu.Watanzania sasa tunaishi kwa imani.Wale wasioitunza imani matunda yake wewe ni shahidi.Wanatusaidiaje na elimu waliyonayo?Tumezidi kuwa wakiwa na maskini katika nchi tuliyozaliwa na tutakufa masikini.Sasa hivi nimemaliza kidato cha sita na nimekosa nafasi ya kuendelea na Elimu ya juu.Nifanye nini katika jamii inayonizunguka nisaidike kimaisha?Kila ninapokwenda kuulizia kazinaambiwa niwe na Expirience tena ya miaka mitatu hadi mitano.Hivi Professa amezaliwa hapa Tanzania?Huu sio ndiyo mwisho wa Maisha yangu?Nafikiri ni muda wa viongozi kuangalia mfumo mzima wa elimu iliumjengee mtu uwezo wa kujiajiri pindi unapomaliza kiwango chchote cha elimu.
Kuna haja au nia ya ndani ya kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu kutamani maendeleo.Ndiyo maana kila mwaka tunachagua viongozi wapya tukitegemea mabadiliko lakini hali huwa tofauti.Zamani shule za msingi zilikuwa na elimu ya ufundi,mitaala hiyoirudishwe ili itujengee uwezo wa kujitafutia Maisha.Professa akumbuke maandiko yanasema "Mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataisau mpaka kufa"Elimu ya Mungu ni muhimu sana katika kizazi hiki kilichopotoka.Kinaprofesa wangekuwa na hofu ya MUNGU ndani mwao wasingekula wala kutoa rushwa.Ni vigumu sana wao kushughulikia maendeleo ya nchi hii kwa dhati kwani wao maisha haya na adha hii hawaionji.Watoto wao wanasoma na kutibiwa nje hivyo suala la kiwango cha Elimu au Afya bora hilo wao haliwahusu.Kwenye majukwaa watasema tena kwa ufasaha na kupangilia maneno kwa ustadi ila utekelezaji huwa ni ndoto.Tunamshukuru Mungu ametupa Rais mwaminifu ,mtanashati,mcapa kazi na mtu anayejali ila cha kusikitisha amezungukwa na mapapa.Amekuwa tone la maji katika bahari,lakini bado tuna Imani naye.Msanii mmoja wa muziki alisema"Time will tell if not actions"
Tumechoka na hali halisi ya maisha hasa kwa watu wenye familia.Umri wa kuishi umepungua kutokana na mshinikizo wa hali ngumu ya maisha.
Mimi napinga ujambazi na matendo maovu lakini ni siku ya tatu sijala wala kunywa chochote na mwili umebakiza hatua za mwisho.Sina kazi kibarua changu cha zege nimesimamishwa twasubiri kuitwa tena mwezi ujao,elimu yangu darasa la saba,naomba ushauri nifanye nini niweze kuishi?Kumbuka Dunia ipo mbele yangu na vishawishi vyote!
* Comment by Mollel
* Date Tuesday, December 29, 2009
View Original Story