/td> Tafuta DHWTangazaTuandikie

Darhotwire.com haitahusika na maoni ya msomaji yeyote aliyotuma katika ukurasa huu kuhusiana na story zetu.

Kibarua cha mlinzi mashakani...baada ya kujibizana na Ngejeja ATM


Ngeleja huo ni ushamba, ulimbukeni na ujinga wa hali ya juu. Sasa wewe tutrakutofautishaji na mtu wa kawaida, kiongozi sio mtu wa kupenda wananchi wake wapate shida, bali wawe na furaha. Sasa bwege wewe unataka tena kwa kiburi cha hali ya juu eti jamaa aachishwe kazi. Kuweni na mtizamo wa haki. Kukwambia kwamba kuna watu wasubiri nje kuchukua pesa zao kama wewe ulivyokuwa unachukua pesa zao lilikuwa kosa gani. Fungua benki yako ambayo utakuwa unasimama na kupiga simu masaa ishirini na manne. Kwa kweli nimesikitiswa na kitendo hicho, baada ya kupongeza kazi nzuri ya huyo jamaa wewe unaponda na kusema apate adhabu kwa kosa gani jamaani. Watanzania tukiendelea kunyamazia mambo kama haya ni hatari. Watanzania ni watu wenye upendo na daima tunakuwa na huruma sio ubosi, huo si utanzania. Kweli washamba mkiwapa vyeo wanajiona kwelikweli. NI kitendo cha kipumbavu kumwambia mtu WEWE UNANIJUA-kwani umekuwa MUNGU

* Comment by Rushubirwa Gilbert
* Date Friday, January 8, 2010
View Original Story

Kama kweli hivyo ndivyo ilivyokua.huyo kijana hapaswi kufukuzwa kazi.na kama akifukuzwa basi huyo waziri wenu nae mungu atamuadhibu tena adhabu kali kuliko kawaida

* Comment by racheal
* Date Friday, January 8, 2010
View Original Story

Nafikiri huyo mlinzi alitimiza wajibu wake kikazi nakama hatapatiwa haki sawa kutakuwa hakuna maana yauzalendo. Kila mtu anaheshimu kazi inayompatia riziki, naniwajibu wakila mfanyakazi kuheshimu nakufanya kazi yake kama anavyotakiwa kufanya. Sioni kama nisahihi kutumia cheo au madaraka kunyanyasa wengine. Nafikiri huyo waziri angetumia busara yakupisha kwanza wengine aendelee namaongezi yakwenye simu baadaye akimaliza ndiyoachukue pesa angepungukiwa, zaidi angeonekana ana busara sana. Ukweli nikwamba ATM nisehemu yakuchukulia fedha nasiyo pakuongelea na simu au iwe CALLBOX.

* Comment by Abby
* Date Wednesday, January 13, 2010
View Original Story

nimeisoma habari hii....inavuta hisia kwa yeyote mwenye utimamu wa fahamu zake.

kama yaliyoandikwa ni ya kweli, basi sioni tatizo juu ya utendaji wa Mnaku katika kutekeleza majukumu yake.

Mnaku yuko right kwa sababu lengo la ajira za watanzania ni kuhudumia umma. maana ya umma ni pamoja na watu wasio na nyadhifa kubwa kama za muheshimiwa Ngeleja.

umuhimu wa muheshimiwa Ngeleja unajulikana wazi kutokana na wadhifa wake. anawajibika kutumikia wananchi wa kada zote bila ubaguzi, anawajibika kuhakikisha kuwa nishati inakuwepo ya kutosha kwa ajili ya matumizi salama ya watu wote wa nchi hii, anawajibika pia kuhakikisha kuwa madini ya nchi yetu yanalinufaisha taifa kwa ujumla.

hayo ni ya Ngeleja kama waziri.......

Mnaku kama mlinzi na yeye ana majukumu, nna uhakika na hili alilolifanya kwa muheshimiwa ni moja ya majukumu yake kwani. Kuongea na simu si tatizo sana ila kama ni kwa muda mrefu, huwa ni kero. kwa heshima ya muheshimiwa waziri kuna uwezekano alikuwa anaongea na simu katika kutekeleza mambo ya kitaifa...kama ni hivyo na yeye alikuwa sahihi.

nionavyo mimi pengine tatizo ni sehemu ambayo mheshimiwa alikuwepo. Hebu fikiria kama umati (msururu) wa watu ulikuwa nje ukisuburi huduma ya ATM, watu hawa walikuwa wanaudhika kwa kiasi gani!

wengine wanataka kwenda hospitali, wengine kulipia ada, wengine kulipia bili za umeme n.k. kuwachelewesha watu hawa ni kupunguza kasi ya maendeleo....

mheshimiwa ni mwenye sura ya upole sana, sikuamini kama jambo hili amefanya yeye otherwise kuwe na sababu nyingine tofauti na iliyoandikwa hapa, lakini kama yalionadikwa ni kweli, basi angeendelea kuwa mpole tu na kumtaka radhi bwana Mnaku kiaina, na watu wangemwona muungwana na kumpenda zaidi.

namuomba mheshimiwa Ngeleja amsamehe bwana Mnaku kwani lililojitokeza ni jambo la kawaida katika utendaji wa kila siku wa shughuli za kibinadamu. Waziri alikuwa na majukumu yake na Mnaku alikuwa na majukumu yake, inafanana na meno kunywani, yote yanawajibika bila kuumizana, siku moja ukitokea ugomvi wa meno, basi kitakachoumia ni ulimi. Ulimi hapa ni familia ya bwana Mnaku (mke, watoto na wanaomtegemea)

Mungu ibariki Tanzania.

* Comment by shabby
* Date Friday, January 8, 2010
View Original Story

nadhani viongozi wetu wanapenda kutukuzwa sana.kama asipomsamehe huyo mlinzi akifukuzwa kazi itamsaidia nini huyo mkuu.sawa mwenye nguvu mpishe lakini mungu ndie anaetoa hukumu ya kweli.

* Comment by pili
* Date Friday, January 8, 2010
View Original Story

SIONI KOSA KUBWA KWA MLINZI KWANI BINADAMU WOTE NI SAWA HATA KAMA NI WAZIRI, KWANI KUNAUBAYA GANI KUWAPISHA WENGINE?

* Comment by MTANZANIA MWEMA
* Date Friday, January 8, 2010
View Original Story

Inaonyesha wazi kwamba ufisadi hautoisha bongo na utazidi kuota mizizi, Mtu hata ukiwa kiongozi haimaanishi kuwa ndio wakati wa kufanya unavyotaka bila kujali wengine na pia kitendo cha kutisha watu kwa nafasi uliyo nayo ni haramu kabisa katika jamii, kwanini udharau watu ambao ndio waliokuweka hapo ulipo. eti "hujui nafasi yangu". who are you? vingozi kama hawa wanaolewa madaraka watapelekea kutia watu hasira. Tumechoka
kwa uwezo wa mungu azabu yoyote atakayo pewa mlinzi huyu, basi na waziri pia impate kama hiyo, amin.

* Comment by mkereketwa
* Date Saturday, January 9, 2010
View Original Story


Kwa mtazamo wangu mlinzi alikuwa sahihi, kumuomba Ngereja apishe wateja wengine,Badala ya kuendelea kuongea na simu wakati watu wanasubiri kwenye mstari. Na hii ni huduma kwa jamii, ambayo haiangazi cheo au wadhifa wa mtu katika kuitumia. Aliyewahi ndio anaanza na kwa kuzingatia muda. Kwa msomi kama Ngereja, haimpasi kuchukua zaidi ya Dakika 1 au 2 kwenye ATM machine. After all its not a BIG DEAL mpaka kuanza kuweka vikao vya kutafuta ukweli na ana makosa kati ya MLINZI VS NGEREJA, Wakati anamajukumu mengi yanayomkabiri.

* Comment by Jafferson
* Date Saturday, January 9, 2010
View Original Story

Waziri anatakiwa kuwa mfano kwa jamii.Kitendo alichofanya waziri Ngeleja kinatakiwa kilaaniwe na kila mtanzania mpenda maendeleo.Huu mtindo wa ndio bosi uachwe mara moja. UKija kutumia mashine wewe ni customer like any other. Hivi mtamlaumu mtu anayetaka kuishi maisha yake nje ya nchi kutokana na upuuzi huu.Hata senator wa Marekani hathubutu kuact kama huyu. Yaani Tanzania imenichosha na upuuzi hivi tumelaaniwa. Kweli hamna watu wakumtetea mlinzi kama huyu. Tunataka watu kumi wenye ushupavu huu.I am getting ready to say bye bye Tanzania.Kunyanyaswa hivi kunatofauti gani na enzi za mkoloni.

* Comment by Amini
* Date Sunday, January 10, 2010
View Original Story

Watanzania msiwe washamba kiasi hicho.
Wengine mnahukumu tayari wakati stori ni ya kupika wala haina mwandishi wala authority.

Ni kipimo kuona kama mko makini hivyo. Magazeti mangapi yameandika au nani ameiandika si Nipashe wala gazeti jingine.
Kweli vyombo vya habari vikiandika jana ulitukanwa utajibu nawe kwa tusi bila kujua ukweli. Acheni ushamba.

* Comment by Nanne Welsy
* Date Monday, January 11, 2010
View Original Story

Waziri amekosea kwanza kwa nafasi aliyonayo na kimaadili hatutegemei mtu mzima akatukana matusi tena hadharani. kama mlinzi ataachishwa kazi basi waziri atakuwa amemtendea mlinzi ndivyo sivyo kwa sababu mlinzi aliona kosa ambalo lipo wazi na ni wajibu wake kusaidia wateja wa aina km ya waziri. waziri akubali kosa na sio kutumia nafasi aliyonayo kutesa wengine.

* Comment by jacque
* Date Monday, January 11, 2010
View Original Story

Kwani kunakosa gani kiongozi kuambiwa atoke ama kumbushwa kwamba kuna wateja wengine wanahitaji kutumia hiyo mashine ili wapate huduma wanayoiitaji? kwa mfano hapo wote wangekuwa wa lank moja ingekuwaje. Mimi naona unapokuwa kiongozi lazima uwajali wananchi na sio kujijali wewe, tena yeye angepaswa kuwasubiri wananchi wapate huduma na yeye aje nyumba yake. Kitendo ya kujibizana na Ultimate Security haioneshi picha nzuri.

Je ndivyo hivyo anavyo tupeleka na Uwaziri wake.

Nkwabi

* Comment by N.T. Kisanga
* Date Monday, January 11, 2010
View Original Story

umekua utaratibu kwa viongozi wetu kutumia madaraka yao hovyo,sidhani kama ni busara kuambiwa jambo ambalo hata yeye angekua kwenye foleni lingemsaidia afu anajibu jeuri kisa ye ni waziri...WHO IS WAZIRI IN TERMS OF SERVICES??KIJANA HATAKIWI KUHOFIA AJIRA YAKE KWA KUTIMIZA WAJIBU..NA WAZIRI ASITISHE WATU KWA KUPEWA CHEO CHA KISIASA!!!AFANYE KAZI BADALA YA KUANZA KUTUMIA MUDA WA KAZI KUTUKANA WATU...NGELEJA UMENIKERAAAA SAAAAANAHHH!!!!!

* Comment by mtossah
* Date Thursday, January 14, 2010
View Original Story

kwani waziri hakosei au akikosea asiambiwe kisa waziri.kwanza huyo waziri ni mbinafsi utaongeaje na simu ndani kwenye ATM while anaona wengine wanasubiri.uonevu tu huo jamani.Mungu atakulipia kijana you did gud job

* Comment by thanks
* Date Saturday, January 16, 2010
View Original Story


Archive:

Copyright © 2010 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.