Darhotwire.com haitahusika na maoni ya msomaji yeyote
aliyotuma katika ukurasa huu kuhusiana na story zetu.
Mtoto adaiwa kufa baada ya kupinga kuolewa
Masikini, kumbe bado kuna jamii ya isiyo na dini na hawana utu kabisa, hawana tofauti na mnyama. Hizi ni zama za sayansi na tecknolojia na suala la elimu limepewa kipaumbele hasa kwa watoto wa kike. Sasa huko umasaini naona bado wamelala usingizi tena wa pono. Jamani serikali iko wapi? Hebu washughulikieni haraka wote waliosababisha ukatili huo wa kijinsia, ili liwe fundisho kwa wale wote wanaoendeleza mila za kishenzi. Mungu aliumba kila kiungo cha mwanadamu akiwa na maana yake, kwa nini wao washindane na Mungu? Masikini Mungu ailaze roho ya marehemu Winifrida mahali pema peponi- Amina!
* Comment by Martina Mturano
* Date Monday, January 11, 2010
View Original Story
Kweli habari hii insikitisha mno,na inaonyesha ni jinsi gani adhabu haitolewi ya kutosha ndio maana mambo haya hayaishi.Tanzania ya leo kweli bado kuna watu wanaowalazimisha watoto kuolewa,na kuwatandika viboko,tena kwa kuwafunga kwenye mti?jamani hapo mahali hakuna hata serikali ya kijiji?au uhuru wa jamuhuri ya kumlinda kila mtu hapo kijijini?Hii inaonyesha kuwa bado tuko mbali sana na bado ule ukoloni upo tena hadharani,waliofanya kitendo hicho wachukuliwe hatua za kisheria ili liwe fundisho kwa wengine wao.
* Comment by Maria Changa
* Date Tuesday, January 12, 2010
View Original Story
Nimesoma habari hii nimeumia sana.kitendo cha kumchapa msichana mdogo mpaka kufa.fikiria, alivyokuwa akilia kwa uchungu,lakini bado alikuwa akipigwa.Mungu mpokee binti huyo mdogo aliyekosa mtetezi siku hiyo kwani naamini wewe pekee ndiye mwamuzi, ndiye mtetezi wa wanyonge.in jesus christ i pray.
* Comment by joyce
* Date Wednesday, January 13, 2010
View Original Story
kuna haja ya watendaji wa kosa hili kushughulikiwa mara moja ili dunia iwe mahari pazuri pa kuishi kwa kila mtu. Watoto, wanawake na wanaume.hali hii ikiachwa, baadhi tu ya watu watakuwa nafuraha na kujiona wanahaki ya kufanya chochote na wengine kubaki wasijue kama kesho yake wataiona
* Comment by Jacqueline
* Date Friday, January 15, 2010
View Original Story
may god blessing her!
amekufa kutetea haki yake ni heshima kubwa !
ni aibu kuwa tz hadi katika karne hii kunatoka mambo kama hayo ya kiajabu, nTUMAI VYOMBO vinavyohusika vitawakamata waliohusika na kupewa adhabu ya kifo!
* Comment by mrusi halisi
* Date Friday, January 15, 2010
View Original Story
may god blessing her!
amekufa kutetea haki yake ni heshima kubwa !
ni aibu kuwa tz hadi katika karne hii kunatoka mambo kama hayo ya kiajabu, nTUMAI VYOMBO vinavyohusika vitawakamata waliohusika na kupewa adhabu ya kifo!
* Comment by mrusi halisi
* Date Friday, January 15, 2010
View Original Story