Share |

17 na ufukunyuaji wa tiketi ya Olimpiki

Kwani michuano hiyo inatarajia kushirikisha Mabondia kutoka nchi mbalimbali, na yatawika hapo Aprili Morocco.

Naye Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema Mabondia hao ambao siku ya Jumatano na Alhamisi walishiriki mapambano ya mchujo, kwenye Uwanja wa ndani siku ya Jumanne watakutana na Makocha pamoja na waamuzi kwa dhumuni la kuzungumzia kambi hiyo.

Si lingine bali ni lile Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), siku chache zilizopita iliteuwa mabondia 17 watakaoingia kambini kujiandaa na mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki itakayowika London, Uingereza hapo badaye ndani ya mwaka huu.

Mabondia ni pamoja na John Christian na Said Pume (lightfly), Abdalla Kassim na George Costantine (fly), Emilian Patick na Undule Langson (bantam), Dennis Martine na Fabian Gaundence (light), Victor Njaiti na Hamisi Kitenge (lightwelter).

Wengine ni Mohamed Kibambai (welter), ambaye atashiriki peke yake katika nafasi hiyo, huku wengine ni Seleman Kidunda na Abdul Rashid (middle), Moris Mhina (lightheavy), Haruna Sanga na Nuru Ibrahim (heavy), na Maximialian Patrick (superheavy).

Kwani makocha watakaoinoa timu hiyo wanatarajiwa kutangazwa kesho Jumanne baada ya kikao cha BFT, Chama cha Makocha na kile cha Waamuzi wa mchezo huo.

Alisema kuwa vyama hivyo viwili lazima vishirikishwe katika mchakato mzima wa kuteua makocha ili kupata watu muafaka.

Ni mingi Tanzania haijashiriki katika Michezo ya Olimpiki baada ya mabondia wake kushindwa kufikia viwango vilivyoweka ili kushiriki katika mashindano hayo.

Na ni zaidi ya Sh milioni 200 zilikuwa zinasakwa na BFT ili kuiandaa na kuipeleka timu hiyo nchini Morocco, lakini hadi sasa hawajapata wadhamini wowote wa kuwasaidia.