Msanii Ali Kiba a.k.a Ali Ulaya ambaye nyota yake iling'ara vyema kimuziki kipindi cha mwaka jana, amechana live kuwa huenda mwaka huu akabadili style ya utokaji.
Kwa mujibu wa Ally amekuwa akifikiria kuachana na style ya kutoa albam ili aanze kutoa Single moja moja ambazo anaamini zitaweza kuuza vizuri zaidi.
Hata hivyo amesema hataweza kukurupuka katika hilo, hivyo ameanza utafiti kuona madhara na uzuri wa jambo hilo kabla ya kufanya maamuzi.
“Nataka kufanya hivyo lakini siwezi kuchukua maamuzi ya haraka kwani kila kitu kinahitaji uchunguzi ili kujua madhara yanayoweza kutokea hapo baadae,” alisema.