Katika hali ambayo sio rahisi kuamini Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Bw.Augustino Mrema a.k.a Mzee wa Kiraracha, amesema nyongeza ya posho za wabunge kutoka sh. 70,000 hadi sh.200,000, haiendani na hali halisi ya uchumi wa Mbongo hivyo kama zitatolewa, zitamchonganisha mbunge na wananchi waliomchagua.
Mrema alisema msimamo wa chama hicho ni kupinga nyongeza hiyo kwani Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo ni bora fedha hizo zikatumika kuharakisha maendeleo ya sekta mbalimbali.
Kwa mujibu wa Mzee wa kiraracha,wazo la kuongeza posho za wabunge limetolewa kwa kukurupuka bila kuangalia madhara yanayoweza kumpata mbunge husika.
“Mtu aliyetoa wazo hili amekurupuka, fedha hizi ni nyingi sana bora ingekuwa sh. 100,000, kimsingi nchi yetu ina matatizo mengi, baadhi ya watumishi serikalini wanalipwa mishahara midogo hivyo fedha hizi wangeongezwa wao pamoja na walimu,” alisema.