Si mwingine bali ni yule nyota wa zamani aliyewahi kuiletea Tanzania Medali mbalimbali, zikiwemo za dhahabu alisema kwamba amejitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuutaka Urais wa chama hicho ili kuondoa ukame wa kupatikana kwa Medali uliyolikumba Taifa.
Kwani Kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), kwa nafasi ya wagombea Urais kimezidi kupamba moto baada ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho na Mwanariadha mahiri wa zamani Kanali Mstaafu Juma Ramadhani Ikangaa kujitosa kuchukua na kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa.
Kwa kipindi cha muda mrefu mchezo wa riadha umepoteza mwelekeo, kutokana na kutokuwepo mipango madhubuti ya kuwawezesha wanariadha wa Tanzania kufurukuta katika medani ya kimataifa.
Kwani atatumia uzoefu wa miaka 10 aliyowahi kuwa katibu mkuu wa chama hicho na umaarufu wake kimataifa katika medani ya riadha, kushawishi wafadhili wa ndani na nje ya nchi kusaidia maendeleo ya mchezo huo.
Ikangaa mwenye rekodi ya kushinda mbio za kimataifa za New York City Marathon mwaka 1989 akitumia saa 2:8.1 na kutwaa medali ya dhahabu.
Alisema umefika wakati kwa wajumbe wa chama hicho kuleta mabadiliko ya lazima ili kuuokoa mchezo huo, ambapo anatarajiwa kuweka mipango ya muda mfupi, kati na mrefu ili kufanikisha ndoto zake kurejesha hadhi ya riadha hapa nchini.
Kwani nafasi hiyo ya urais inawaniwa na wagombea wengine ambao ni pamoja na Rais anayemaliza muda wake, Francis John, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha, Henry Nyiti huku ukatibu mkuu ukiwaniwa na John Manyama, Mujaya Suleiman Nyambui na John Bayo, ambapo ukatibu msaidizi waliojitosa ni Ombeni Zavala na Julius Musomi.