Mwanadada mwenye kila ina ya mbwembwe na ambaye aliibukia kwenye shindano la Bongo Star Search, Baby Madaha, amejiunga rasmi kwenye Kundi la TMK Wanaume Halisi ambalo linaongozwa na Juma Kassim Ally Kiroboro ‘Sir Nature’.
Kujiunga TMK kumethibitishwa na mwanadada huyo pamoja na kiongozi wa kundi hilo Juma Nature.
Staa huyo alipoulizwa alikiri kufanya kazi na TMK Wanaume Halisi na kuongeza kwamba mwaka huu ameamua kujipanga vyema zaidi ndiyo maana ameungana na vichwa vya kiumeni.
Kwa upande wa Nature, alijibu: “Unauliza maembe kibada? Baby Madaha ndiye first lady wa Halisi. Tumemchukua kwa sababu anaweza kazi.”aada ya kumaliza msimu wa BSS, Baby alifanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini alipotoa ngoma yake inayokwenda kwa jina la Amore, ilimtambulisha vema.