Baada ya barua ya Zitto kabwe ya kutaka aondolewe ktk utaratibu wa kulipwa posho kukataliwa na Spika wa Bunge la Tanzania mama Anna Makinda huku akienda mbali zaidi kwa kusema ambaye hatasign kitabu cha mahudhurio kwa mikutano mitatu mfululizo atafukuzwa mjengoni,Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini,amesema kuwa yuko tayari kufukuzwa aende kulima au kuvua dagaa, kuliko kuzichukua.
Kauli hiyo ya Spika Makinda inakuja siku moja baada ya wabunge wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, kusema kuwa leo watawasilisha nakala ya barua kwake na kwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo kuwa wanataka posho zao zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo Mkoa wa Kigoma.
Kauli ya Bi. Makinda ambayo sasa inaonekana kutaka kuwabana kisheria wabunge ambao wameshaamua kuzikataa posho hizo.
Akizungumza jana ktk maeneo ya bunge, Spika Makinda alisema "Hili suala liko kisheria, mbunge asiposaini posho katika mikutano mitatu mfululizo anahesabika kuwa hayupo, hivyo anafukuzwa bungeni, kwa hiyo sisi tutawahesabia tu...lakini pia hili suala la mshahara wa mbunge linakuzwa, hizo milioni saba zinatoka wapi...mshahara wa mbunge ni milioni 2 na nusu...kabla ya kodi, kisha kila mwezi anakatwa laki tisa za mkopo wa gari, anakatwa kodi laki tano," alisema Spika Makinda kwa kifupi.