Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua rasmi huduma ya kununua mafuta ya gari kwa kutumia huduma ya Airtel Money katika vituo vya GAPCO.
Kwa mujibu wa kampuni hilo lengo la kuanzisha huduma hiyo ni kuhakikisha huduma ya Airtel Money inakuwa suluhisho la kudumu kwa mahitaji ya kila siku kwa wananchi wote na wateja wao.
Kwa kuanzia huduma hiyo itapatikana katika vituo vya GAPCO Dsm vya Sasa kazi-Mtoni Mtongani, GAPCO Banana-Gongo la Mboto na GAPCO-Barabara ya Samora huku wakiahidi kuwa baada ya miezi miwili ijayo watakuwa wamesambaza huduma hiyo katika kwa vituo vingi zaidi.