Share |

Hata sisi tunastahili kupewa Tuzo hizo

Aliamia mashujaa akitokea Twanga Pepeta, alisema hayo kwenye semina maalumu iliyoandaliwa na wandaaji wa tuzo hizo kwa wanamuziki.

Hayo yalisemwa a mwanamuziki wa Bendi ya muziki wa dansi ya Mahujaa, Charles Gabriel ‘Chalz baba’ huku akiwalalamikia waandaaji wa tuzo za muziki za Kilimanjaro kwamba wamewasahau  wanamuzi wa dansi katika baadhi ya vipengele vya kuwania tuzo hizo.

Alisema kwamba kunavipengele vingi ambavyo anamuziki wa dansi hawapo, kwa mfano mtumbuizaji bora wa kume na kama kunawasanii wanaotumbuiza ni wanamuziki wa dansi lakini wao hawawekwi.

“Haya Muimbaji bora wa kiume, yale yake yamejirudia tu hivi jamani kweli watu wa dansi hakuna muimbaji kweli? Na hata kwa upande wa wanawake ni hivyohivyo, haya mtunzi bora wa mwaka, wanamuziki wa dansi hakuna majina ni yaleyale yanajirudia,” alisema.

Naye mwanamuziki mwingine wa dansi kutoka bendi ya Mapacha Watatu, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ alisema katika kuwania tuzo hizo wahusishwe wanamuziki wakongwe.

 “Kuna Kina King Kkiki, Msondo, Sikinde, njenje wazee wetu wale wapewe nao vipengele vya kushindana, kwa kifupi wazee wetu wanatengwa”.