Hatimaye Ruge mutahaba na Mh Joseph mbilinyi (Sugu) leo tarehe 21/02/2012 wamemaliza tofauti zao baada ya kufanyika kwa vikao mbali mbali chini ya Wapatanishi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Hili litakuwa tukio la aina yake baada ya mtu 2 hizi kuwa kwenye ugomvi uliodumu kwa miaka 2.
Baadhi ya picha hapo zinaonyesha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati wakiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili.
Moja ya maneno aliyonukuliwa Sugu akiongea mbele ya waandishi na kuwafurahisha wengi ni pale aliposema " VITA LAZIMA IWE NA MWISHO UNLESS KAMA HAINA MALENGO"