Share |

Kamwe hatutaidharau Ethiopia

Kocha huyo alisema kwamba kuna tofauti na wengi wanavyofikiri Ethiopia ni timu ngumu, kwani inacheza kwa uelewa mkubwa na hivyo maandalizi yanahitajika mapema.

Si mwingine bali ni yule Kocha Mku wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Soka 'Twiga Stars', Charles Mkwasa alisema kwamba hawataidharau Ethiopia kwa sababu nayo ni timu nzuri.

Timu ya Ethiopia iliwafunga Misri mabao 4-0 nyumbani na kufanikiwa kuvuka hatua ya mwisho ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika ambapo watacheza na Twiga Stars Mei 25.

Kwenye mchezo wa awali uliochezwa Cairo wiki mbili zilizopita Misri ilishinda kwa mabao 2-0.

Akizungumza na 'Habarileo', Mkwasa alisema kuwa tofauti na wengi wanavyofikiri Ethiopia ni timu ngumu inayocheza kwa uelewano mkubwa na hivyo maandalizi ya mapema yanahitajika.

“Wanapenda sana kumiliki mpira, wanacheza kitimu, haitakuwa rahisi kuwafunga Ethiopia tofauti na wengi wanavyofikiri,” alisema Mkwasa.

Alisema anaifahamu vizuri Ethiopia kwani waliwahi kukutana nayo huko nyuma na kuwafunga mabao 3-1 nyumbani kwao kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa marudiano na kuitoa timu hiyo mashindanoni.

Alisema kwamba wengi walifikiri Misri ingepita kwa sababu nchi hiyo inachukuliwa kuwa miongoni mwa nchi kubwa kwenye mchezo wa soka barani Afrika, lakini hali imekuwa tofauti na hivyo watu wanapaswa kujua kuwa Ethiopia sio timu rahisi.

Alisema kama kocha anaiandaa timu yake kukabiliana na timu yoyote bila kujali ubora au udhaifu wa timu hiyo na kwamba hataidharau Ethiopia watakapokutana nayo Addis Ababa
ambapo mchezo wa kwanza utachezwa huko.

Watanzania kuichangia timu hiyo ili iweze kuingia kambini mapema kujiandaa na mchezo huo muhimu, ambapo kama watashinda watafanikiwa kufuzu kwa fainali zake zitakazofanyika Equatorial Guinea Novemba mwaka huu.