Share |

Kanumba na mkazo wa Elimu kwa Wasanii

Kwani watayarishaji hao wa Filamu wamekuwa wakilazimika kuwatumia Wasanii, wasio na sifa katika fani hiyo ya Uigizaji na kusema kwamba amekerwa na utovu wa nidhani wa baadhi ya wasanii.

Hayo yalisemwa na Muigizaji nyota na pia ni Mtayarishaji Mahiri wa Filamu Swahiliwood, Steven Kanumba amewahimiza wasanii kujiunga na vyuo vya Filamu vinavyoanzishwa nchini badala ya kukimbilia kuigiza moja kwa moja.

Alisema ni  vema wakajiunga na vyuo vinavyofundisha fani ya uigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza, sanaa bila elimu ni sanaa dumavu.

Kanumba alisema amebahatika kusafiri kwenye nchi kadhaa, na kuamua kujiendeleza hata kama una kipaji mara nyingi anapata wakati mgumu kila asubuhi anapoamka na kuwakuta vijana wakimngoja nyumbani kwake huku kila akisistiza kuwa yeye ana kipaji na anahitaji kufanya kazi na mimi, lakini ukimpa nafasi hali inakuwa tofauti na maongezi yake.

Anasema hali ya sasa ya Sanaa ya Filamu inakabiliwa na changamoto nyingi hasa baada ya maigizo kupunguza msisimko wake katika televisheni, jambo ambalo watayarishaji wanajikuta wakiwatumia wasanii ambao hawajawahi kupitia katika vikundi vya maigizo ambao wanaamini kuwa wanafuatwa kwa sababu ya urembo wao au umaarufu, hivyo kukosa uchungu na sanaa.

Kanumba alisema kwa wasanii ambao hawajapitia kwenye makundi ya maigizo ni shida, ndiyo maana tunalalamikiwa sana kuwa wasanii tumekosa maadili, lakini si wote.