Share |

Kati ya Stars na Congo nani kupengwa kamasi?

Kwa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, mechi hiyo itachezwa katika muda huo ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kuhudhuria mchezo huo ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kumiminika kwenye mchezo huo.

Ni ile mechi ya kirafiki baina ya Timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapigwa siku ya leo kuanzia saa 11:00 jioni ndani ya Uwanja wa Taifa hapa Jijini.

Kwa ilivyoada mechi za soka huanza saa 10:00 jioni kwa siku za mwisho wa wiki na sikukuu au saa 10:30 jioni kwa siku za kazi na mara chache huchezwa nyakati za usiku.

Siku ya leo Alhamisi ni siku ya kazi kwa hiyo, wameamua waucheleweshe mchezo, ili watu wakitoka kwenye shughuli waje uwanjani.

Mbali na hilo kiingilio kwenye mechi hiyo ya leo kitakuwa ni Sh. 2,000 (kwa viti vya kijani na bluu), Sh 5,000 (vya rangi ya chungwa), Sh 7,000 (VIP C), Sh 10,000 (VIP B) na Sh 15,000 (VIP A).

Taifa Stars na DRC zinatumia mechi hiyo kunoa wachezaji wao kabla ya mechi zao za mchujo kuwania tiketi za fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.