Share |

Monalisa ndani ya Pastor Myamba Trial

Amecheza kama mke wa mtu yaani mke wa  mchungaji, kwenye filamu kali yenye kusisimua ya Pastor Myamba Trial na ni filamu yenye kuelezea mitihani ambayo uwakabili baadhi ya wachungaji kwenye nyumba zao pindi wanapojikuta wakipata shida baada ya familia zao kuwa kwenye hali ya utukutu kama ilivyokuwa kwa Pastor Myamba.

Ni yule Muigizaji Mahiri kwenye sanaa ya filamu ya Bongo Yvonne Cherryl (Monalisa), ndani ya filamu hiyo ameweza kuigiza kama mke wa mchungaji.

Na Mtayarishaji wa filamu hiyo ni Mkurugenzi wa Born Again Production Emmanuel Myamba 'Pastor Myamba', anaamini kwamba kupitia filamu hiyo watumishi wengi wa Mungu wataipokea vizuri na kuwa ni sehemu ya fundisho kwenye jamii.

Pastor Myamba alisema wanaamini kuwa familia zao huwa salama, kwa kufuata misingi ya Mungu kumbe kuna siri ndani yake ambayo mzazi mmoja anaweza kuwa hajui chochote.

“Kama ilivyo katika Pastor Myamba Trial Monalisa anaruhusu vijana wangu ambao ni watoto wake, kujihusisha na tabia za ajabu ajabu kama kucheza mayenu, kuwa na tabia ambazo hazina nafasi katika nyumba ya mchungaji,alisema Pastor Myamba."

Pastor Myamba Trial inawaleta vijana Morgan na Meya ambao ni watundu kweli kweli, na imetayarishwa na kampuni ya Born AgainProduction chini ya meneja wa kampuni hiyo Novatus Mayenje (Nova) huku mkurugenzi wake akiwa ni Emmanuel Myamba (Pastor Myamba).

Kampuni hiyo kwa sasa ipo kwenye kasi ya kuzalisha filamu nyingi sana wakati Pastor Myamba Trial ikiwa tayari vile vile kuna Some time yes, Some time No, nayo ipo tayari.