Kwani Msanii huyo alilitikisa anga la Bongo Fleva miaka ya mwanzoni mwa 2000, alisema baada ya kuamua kurudi kazini kwanza alipania kuachia wimbo wake.
Si mwingine bali ni yule Mkali wa Takeu Lucan Mkenda 'Mr Nice', kwa sasa yupo tayari kuanza kufanya maonyesho baada ya kumaliza kazi ya kutengeneza video ya wimbo wake mpya 'Tabia Gani’.
Hiyo ni baada yakutimiza azima yake ya kuwapa mashabiki wake wimbo huo wa ‘Tabia Gani’ katika kanda za kawaida na baadaye video sasa atafanya mazungumzo na waandaaji wa maonyesho ili wampe nafasi.
Baada ya msanii huyo kumaliza kutengeneza video ya wimbo wangu mpya wa ‘Tabia Gani’, kwa sasa anataka kuanza kufanya maonyesho.
Wimbo huo ameusuka ndani ya Studio ya Lamar iliyopo Kariakoo hapa Jijini, chini ya utayarishaji wa wataalamu Lamar Niekamp na Joseph Dunga.