Alisema kwamba mchango huo ulipatikana kwenye Maonesho ya Mavazi yaliyofanyika Januari 12, ndani ya Hoteli ya Serena.
Si mwingine bali ni yule Mbunifu wa Mavazi na Mitindo hapa nchini, Mustafa Hassanali, aliweza kukabidhi Sh. 5,079, 340 zikiwemo na nguo kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Mafuriko yaliyotokana na Mvua zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana hapa Jijini.
Mbunifu huyo alisema kwamba Maonesho hayo yaliandaliwa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, kwa kushirikiana na yeye.
Alisema wanashukuru kwa kuweza kutimiza mpango wao wa kusaidia waathirika hao wa Mafuriko, minada na Kiingilio cha Maonyesho hayo ya Mitindo waliyoyafanya kwa lengo hilo la kuwasaidia wenzao lilifanikiwa.
Mbali na kuchangia waathirika hao, Onesho hilo lililenga kutambulisha Nguo mpya za Hassanali, ambazo alizizindua mwishoni mwa mwaka jana kwenye nchi mbalimbali zikiwemo Sweden, Angola, Niger na nyinginezo.