Share |

Myamba na mabadiliko kwenye Sanaa ya Filamu

Si mwingine bali ni yule Msanii mahiri kwenye Sanaa ya Filamu za Kibongo Emmanuel Myamba, na ndiye Mwanzilishi na ni Mkurugenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Uigizaji (TFTC) yaani Tanzania Film Training Center.

Chuo hicho hutoa mafunzo mbalimbali ya Filamu za Kibongo ikiwemo Acting, Directing, Editing.

Lengo la Chuo hicho ni kuhakikisha kwamba wanapata kizazi chenye uelewa mkubwa wa mambo ya Filamu, huku wakipata watu wenye ufahamu bora juu ya utengenezaji wa Filamu nchini Tanzania.

Kwani mafunzo hayo ya Acting yameanza rasmi ndani ya wiki mbili zilizopita, katika mazingira mazuri yakiwemo Madarasa yenye kiyoyozi 'AC' cha kutosha.

Images: