Hivi juzi tu tulimsikia Ali Kiba a.k.a Ali Ulaya akisema anajifikiria kuachana na mtindo wa kutoa albam ili aanze kurelase single peke yake.
Leo ni zamu ya bwana mdogo Mr Blue, ambaye nae anasema mwaka huu hatarajii kutoa albamu kwani kwa upande wake hazimlipi.
Blue anasema anapenda kutoa albamu lakini kwa bongo hazina faida kubwa kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine hivyo ni bora tu ale kwa mpango wa single.
"Unajua tunatumia gharama kubwa kutengeneza albamu lakini faida yake inakuwa ndogo kutokana na wizi unaofanywa na watu wasiojali kazi za wasanii".
Blue pia alidodosa kuwa ktk siku za karibuni anatarajia kudondosha pini jipya la kufungulia mwaka analoenda kulifanyia nchini Kenya huku akigoma kutaja jina la wimbo huo mpaka wakati muafaka utakapofika.