Share |

Ni wakati wa kuwa tofauti na wengine!

Msanii Hussein Machozi  amewataka wapenzi na mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa kuwa yuko mbioni kutoka kivingine zaidi.

“Mimi huwa napenda kufanya nyimbo zangu na hasa pale ninapojisikia niandike kitu fulani, huwa naandika halafu namshukuru Mungu kitu hicho kinakubalika katika jamii,” alisema Machozi.

Alisema mwaka huu 2012 amekuja kivingine zaidi ili kuwapa raha mashabiki wake kwa kuwalisha ladha tofauti tofauti na si mlo mmoja kila siku.

Ngoma ya Jela imeanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya runinga na imeonekana kupendwa na watu mbalimbali kutokana na ujumbe uliomo.

Machozi kwa sasa anatamba na nyimbo ya ‘Jela’ ambayo imeonekana kupendwa na mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.