Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema adhabu hiyo inatokana na Kanuni ya 25 ya Ligi na anatakiwa kulipa faini hiyo kabla ya adhabu ya mechi kumalizika.
Si mwingine bali ni yule Beki wa Yanga, Nsajigwa Shadrack Fuso , anayekabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na faini ya Sh500,000 kutokana na kitendo chake cha kumpiga kiwiko, Benedict Ngassa wa Moro United.
Beki huyo husifika kwa soka la nguvu, alifanya hivyo wikiendi iliyopita, katika fungua dimba ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ndai ya Kosa hilo, mwamuzi Hashim Abdallah, alimtoa kwa kadi nyekundu.
Mbali na hilo Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro, amemtupia lawama Nsajigwa huku akisema kitendo chake kiliigharimu Yanga kukosa ushindi katika Mechi hiyo ilikwisha kwa sare ya mabao 2-2.
Kadi yake ndiyo ilitoa mwanya kwa Moro kufunga mabao yao, alisema Minziro.
Mbali na Minziro kusema hayo bosi wake, Kostadin Papic, amemtetea beki huyo huku akisema washambuliaji ndio waliinyima timu ushindi kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi.
Alisema kadi ni kitu cha kawaida kwani wachezaji wengi duniani wanapata kadi nyekundu, Fuso alipotoka bado wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini
hawakuzitumia, huo ni uzembe uliotugharimu.