Ndiyo waandaaji wa Filamu hiyo Robert Mhangwa, imeshindwa kuingia Sokoni jana kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na ukosefu wa DVD yakiwemo na makasha ya kuhifadhia CD hapa nchini.
Ni ile Filamu iliyokuwa ikingojewa kwa hamu sana sokoni na wapenzi wa Filamu za Kibongo, inajulikana kwa jina la Shemeji na imeshindikana kuingia sokoni jana na itaanikwa sokoni hapo Februari 27 mwaka huu.
Naye Mkurugenzi wa Sharks Video Production alisema kwamba tatizo hilo halikuiathiri filamu ya Shemeji pekee, bali na nyingine zote zilizotarajiwa kutoka hivi karibuni, ndiyo maana hakuna kazi mpya zaidi ya zile zinazotolewa na kampuni mojawapo hapa nchini.
Aliongeza kwa kusema kwamba kuwa sasa filamu hiyo itakuwa sokoni, Jumatatu ijayo baada ya kuamua kuzifuata bidhaa hizo nje ya nchi.
Filamu hiyo imeshirkisha nyota wafuatao ni pamoja na Hashimu Kambi, Mshindo Jumanne ‘Papaa Mukubwa’, Ibrahim Mbwana ‘Bad Boy’, Salma Salmini ‘Sandra’, Mzee Msisiri, Raadhani ‘Kishoka’ na wengineo.